Immigration History from Kenya (Swahili) to Victoria
Hapo karne ya Kumi na Tisa (19th Century) Kenya ilijulikana kama Uingereza Africa Mashariki na ilikuwa kwenye kumbukumbu za sensa za victoria mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Moja (1901). Wakati mzaaliwa moja wa Kenya wa asili ya kiume alikuwa mwenyeji wa victoria. Wa Kenya hawakuwa kwenye kumbukumbu za Victoria hadi mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Themanini na Moja (1981). Katika muda huo Kenya ilikuwa imeona mabadiliko makubwa kisiasa, tangu ukiuaji wa uhuru kutoka kwa Uingereza miaka ya Elfu Moja Mia Tisa Na Hamsini (1950s). Kura za kwanza za Legco kwa waafrika zilifanyika mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Hamsini na Saba (1957).
Kuanzia waakazi Mia Tano na ishirini na saba waliokuwa kwenye kumbukumbu za Elfu Moja Mia Tisa na Themanini na Moja. (1981), watu wa Kenya wameendelea kukua wima.
Kufikia 2011, idadi ya watu imekua kwa 155% zaidi hadi 2,851. Wingi wa kenya-waliozaliwa Victoria leo ni Wakristo, 20% ni Wakatoliki na 15% ni Waanglikana. Waislamu ni 14%, huku Wahindi ni 10%. Uwiano mkubwa wa idadi hii ya watu ni wachanga sana: takribani robo moja ya jumla ya idadi ya watu inao umri kati ya miaka mitano na 14.
Kenya inayo idadi kadhaa ya makabila, yakiwemo Kikuyu, Embu, Luo na Maasai na Swahili, na lugha nyingine 62 zinazungumzwa. Lugha kadhaa kati ya hizi zinawakilishwa na mseto wa lugha zinazozungumzwa na Wakenya wanaoishi Victoria. Kiingereza kinazungumzwa na 35% ya Wakenya-waliozaliwa Victoria, huku 26% wanazungumza Kiswahili. Lugha nyingine maarufu ni Dinka, Kisomali na Kigujarati.
Kwa wale walioajiriwa, 52% wanajihusisha katika kazi za usimamizi, wataalamu na kazi nyingine kama hizo, ambapo kundi kubwa zaidi la wataalamu ni uhasibu na wataalamu wa hesabu. Karibu robo ni wafanyakazi wa ukarani, uuzaji na utoaji huduma, ambapo karibu nusu ni wafanyakazi wa utunzaji spesheli na wa kibinafsi. Wafanyakazi wa kazi ya sulubu wanaunda 3% ya idadi ya watu, huku 2% wanayo biashara wanayofanya.
Jumuiya hii inasaidiwa na programu ya lugha ya Kiafrika ya SBS na Baraza la Jumuiya za Kiafrika za Victoria. Jumuiya inasherehekea Jamhuri Day, Uhuru wa Kenya, mnamo mwezi wa Disemba.